TKatiba ya Kigiriki ndiyo sheria ya kimsingi ambayo kwayo huegemezwa sheria zote Ugiriki za haki na wajibu wa raia, muundo na sheria msingi za serikali ya Ugiriki na taasisi zake.
Katika Sehemu ya Pili ya Katiba: Haki za Kibinafsi na za Jamii, ibara ya 5, yafuatayo yametajwa:
- Kila mtu ana haki ya kujiendeleza kimaisha na kushiriki katika mambo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, na maisha ya kisiasa nchini, almuradi mtu huyo asiingilie haki za wengine, Katiba, desturi za watu.
- Watu wote walio Ugiriki wafurahie ulinzi kamili wa maisha yao, heshima na uhuru, bila kujali utaifa wao, rangi, imani, au mwelekeo wa kisiasa; isipokuwa katika hali kama vile ilivyoelekezwa katika sheria za kimataifa. Wageni walioteseka kwa vitendo vya kupigania uhuru wao hawatarejeshwa kwao kuhukumiwa.
- Uhuru wa kibinafsi hauwezi kukiukwa. Hakuna mtu yeyote atasthtakiwa, kukamatwa, kufungwa, au kuwekewa vikwazo kwa vyovyote, ila tu wakati na kwa namna iliyoratibiwa kisheria.
- Hatua zozote za kibinafsi zinazozuia uhuru wa kutembea au kuishi nchini Ugiriki an haki ya kila Mgiriki kutoka au kuingia Ugiriki zitakuwa marufuku. Mikakati kama hiyo inaweza tu kuchukuliwa katika hali za dharura zisizo za kawaida, na kwa ajili tu ya kuzuia vitendo haramu, kufuatia uamuzi wa mahakama ya uvunjaji sheria kwa mujibu wa Katiba.
- Watu wote wana haki ya kulindwa kiafya na utambulisho wa maumbile yao. Mambo yanayohusiana na usalama wa kila mtu dhidi ya hatua za kimatibabu yataelezewa kwa mujibu wa sheria.