Mfumo wa Utawala
Jiografia, Habari ya Idadi ya Watu
Mila, Tamaduni

Sera za uhamiaji

Afya, Kazi, Elimu

Huduma, Taasisi, Ushauri
Uko hapa:  Jiografia – Habari ya Idadi ya Watu / Habari ya Idadi ya Watu

Habari ya Idadi ya Watu

Kwa mujibu wa sensa iliyopita (2011), idadi ya wakazi wa kudumu nchini Ugiriki ni wenyeji 10.815.197. Jumla ya idadi ya wahamiaji inakadiriwa kuwa 10% ya jumla ya watu wote, au watu 1.200.000 Takriban nusu ya wakazi hao ni wakazi wa kisheria ingawa idadi hiyo inahitilafiana pakubwa kufuatia ukosefu wa sera rasmi za uhamiaji na migogoro ya kisiasa katika nchi jirani. Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Uimarishaji wa Utawala za mwaka 2015, idadi ya wakazi wa kisheria kutoka mataifa ya tatu ilikuwa watu 501.875, ambapo asilimia kubwa zaidi (68%) ilikuwa ya Albania, ikifuatiwa nay a Kiukreni (3.6%), Kijojia (3.3%), Pakistani (3.1%), Urusi na India (2.6% kila moja), na Ufilipino (1.9%), huku raia wa nchi zingine wakiwa na asilimia finyu zaidi. Kutoka 2011 hadi 2015, takwimu zinaonekana kupungua, hususan kwa sababu ya mgogoro wa kiuchumi (wakiikimbia Ugiriki, ukosefu wa nyaraka za kisheria kutokana na ukosefu wa ajira/biashara haramu), lakini pia kwa sababu ya mataifa mawili maalum kuwatuma wahamiaji Ugiriki, Bulgaria na Romania kujiunga na Umoja wa Ulaya.


Rudi
Mradi wa 1.4.b/13 ‘Matangazo ya Redio ya masuala kuhusiana na wahamiaji, uzazi, na usambazaji mpana wa vifaa vilivyochapishwa, vya sauti na vielelezo’ ulifadhiliwa 95% na Hazina ya Jumuiya na 5% na Rasilimali za Kitaifa