Hali ya anga katika Ugiriki kimsingi ni ya Mediterenia yenye msimu wa baridi kali na mvua, pamoja na msimu wa kiangazi wenye joto Hali ya anga ya Ugiriki inaweza kugawanywa katika vijisehemu vinne:
Halijoto ni nadra kupita kiasi katika maeneo ya Pwani. Halijoto ya juu huonekana katika tambarare funge na nyanda za juu za nchi kila siku na kila mwaka. Kuanguka kwa theluji ni jambo la kawaida juu ya milima kuanzia mwisho wa Seputemba (kaskazini mwa Ugiriki; na kwa wastani mwishoni mwa Oktoba katika maeneo mengine ya nchi), huku theluji ikianguka katika maeneo tambarare hasa kuanzia Desemba hadi katikati ya mwezi Machi Hata hivyo, katika Florina theluji huanguka hata mwezi wa Mei. Katika maeneo ya Pwani ya visiwa, kuanguka kwa theluji sio kwa mara kwa mara, na sio kipengele muhimu cha hali ya anga. Mawimbi ya joto hasa huathiri maeneo tambarare na mara nyingi huwa katika Julai na Agosti. Hata hivyo, ni vigumu kuwepo kwa zaidi ya siku 3.
Kwa mujibu wa hali ya anga, mwaka unaweza kugawanywa katika misimu miwili: msimu wa baridi na mvua, ambao hukaa kuanzia katikati ya Oktoba hadi mwisho wa mwezi Machi; na msimu wa joto na kiangazi, ambao hukaa kuanzia Aprili hadi Oktoba.
Katika kipindi cha kwanza, miezi ya baridi tele ni Januari na Februari, ambapo kiwango cha chini cha wastani cha halijoto huwa ni kati ya 5-10 °C katika maeneo ya Pwani, kutoka 0-5 °C katika maeneo ya bara, na halijoto ya chini ya sufuri katika mikoa ya kaskazini.
Mvua haidumu kwa siku nyingi, hata wakati wa msimu wa baridi, na anga haibakii na mawingu mengi katika majira haya ya baridi, kam ilivyo katika sehemu zingine duniani. Hali mbaya ya anga mara kwa mara huingiliwa na siku za jua katika mwezi Januari na siku 15 za kwanza katika mwezi Februari, na ambazo zimekuwa zikijulikana kama “siku za Halikoni” tangu jadi. Kwa hivyo, wakati wa kipindi hiki, katika visiwa hasa vya kusini mwa nchi kama vile katika Krete, halijoto yaweze kuzidi nyuzi 18-20, nyuzi 13-14 katika Atika, na nyuzi 9 au 10 katika Thesaloniki. Katika miji mingine kama vile Aleksanduroipoli, halijoto huongezeka kuzidi nyuzi 7-8 katika siku za Halikoni, na kuruhusu theluji ya msimu wa baridi kuyeyuka wakati wa mchana.
Kiwango cha baridi wakati wa msimu wa baridi huwa chini katika Eejeni na Bahari ya Loniani, kuliko kaskazini na mashariki mwa bara ya Ugiriki. Wakati wa joto na kiangazi, hali ya anga huwa imara, anga huwa shwari, jua huangaza zaidi, na hakunyeshi isipokuwa nyakati fupi za rasharasha na ngurumo.
TKipindi cha joto zaidi huwa ni siku kumi za mwisho za mwezi Julai na siku kumi za kwanza za mwezi Agosti, ambapo kiwango cha wastani cha halijoto huwa ni kati ya nyuzi 30 na nyuzi 35. Wakati wa msimu wa joto, halijoto ya juu husawazishwa na ubaridi kutoka maeneo ya pwani ya nchi, na kutokana na upepo wa kaskazini wa kila mwaka unaovuma hasa katika Eejeni.
Majira ya kuchipua huwa ni mafupi, kwa sababu majira ya baridi yaweza kuchelewa, lakini majira ya kiangazi huanza mapema. Majira ya vuli huwa marefu na yenye joto, na wakati mwingine huweza kuenea hadi kusini mwa Ugiriki na visiwani hadi katikati ya Desemba. Katika Atheni, jiji kuu, hali baridi ya anga kwa kawaida huwa kuanzia Novemba na kuendelea, na kisha kuendelea hadi mwishoni mwa mwezi Machi. Baada ya katikati mwa Desemba, maeneo ya mijini huwa na msimu wa baridi, unaoendelea hadi mwisho wa Februari. Tangu siku za mwanzomwanzo za Machi, Majira ya kuchipua hutambulika, na halijoto huongezeka taratibu. Kilele cha baridi katika jiji la Atheni huchukuliwa kuwa kuanzia wiki ya mwisho ya Desemba hadi wiki ya tatu ya Januari. Zaidi hasa, halijoto chini zaidi kuwahi kurekodiwa katika Atheni ni nyuzi -17.1 mnamo Desemba 28, 1938; na halijoto chini zaidi nchini kuwa nyuzi -30. Nyuzi -28 (Kato Nevurokopi) na nyuzi -27 (Putolemaida) zimewahi kurekodiwa pia. Ugiriki inashikilia rekodi ya halijoto juu zaidi katika bara ulaya, ya nyuzi 48.0 katika Atheni, Julai 10, 1977 – hakika, imewahi kuripotiwa kuwa kipimajoto kiliwahi kufikia nyuzi 48.7. Kiwango hiki kilirekodiwa Juali 10, 1977 katika mji wa Elefisina. Viwango vingine vya halijoto juu kurekodiwa ni pamoja na nyuzi 47.5 katika Filadelfeia ya Sasa (Manispaa ya Atheni) mnamo Juni 26, 2007, na Lioni (Atika), siku io hiyo.
Mji | Wastani wa kila mwaka | Jan. | Feb. | Mac. | Apr. | Mei | Jun. | Jul. | Ago. | Sep. | Okt. | Nov. | Des. |
Atheni | 18,1 | 5,1 | 6,5 | 8,7 | 14,6 | 21,3 | 28,1 | 31,0 | 30,4 | 25,4 | 18,1 | 11,3 | 7,0 |
Loanina | 14,3 | 4,7 | 6,1 | 8,8 | 12,4 | 17,4 | 21,9 | 24,8 | 24,3 | 20,1 | 14,9 | 9,7 | 5,9 |
Arita | 17,2 | 8,7 | 9,4 | 11,9 | 15,2 | 19,9 | 24,0 | 26,5 | 26,5 | 23,1 | 18,3 | 13,5 | 9,9 |
Aleksanduroupoli | 15,0 | 5,0 | 5,9 | 8,3 | 13,1 | 18,3 | 23,1 | 25,8 | 25,4 | 21,1 | 15,6 | 10,8 | 7,1 |
Kavala | 15,8 | 6,8 | 7,2 | 9,3 | 13,4 | 17,7 | 23,0 | 26,5 | 26,3 | 22,4 | 17,2 | 11,4 | 8,0 |
Thesaloniki | 15,7 | 5,2 | 6,7 | 9,7 | 14,2 | 19,6 | 24,4 | 26,6 | 26,0 | 21,8 | 16,2 | 11,0 | 6,9 |
Seresi | 15,1 | 3,9 | 6,2 | 9,6 | 14,2 | 19,6 | 24,3 | 26,3 | 25,3 | 21,6 | 15,5 | 9,2 | 5,0 |
Florina | 12,1 | 0,5 | 2,7 | 6,7 | 11,6 | 16,8 | 21,0 | 23,1 | 22,5 | 18,4 | 12,6 | 7,0 | 2,2 |
Kozani | 12,9 | 2,3 | 3,7 | 6,9 | 11,6 | 16,8 | 21,5 | 24,1 | 23,6 | 19,3 | 13,5 | 8,0 | 3,9 |
Larisa | 15,7 | 5,2 | 6,8 | 9,4 | 13,8 | 19,7 | 25,0 | 27,2 | 26,2 | 21,8 | 16,2 | 10,8 | 6,6 |
Volosi | 16,2 | 6,6 | 7,6 | 9,9 | 14,1 | 19,5 | 24,5 | 26,8 | 26,1 | 22,2 | 16,9 | 12,1 | 8,2 |
Agrinio | 17,2 | 8,3 | 9,2 | 11,5 | 15,1 | 20,3 | 24,7 | 27,1 | 26,9 | 23,0 | 17,9 | 13,1 | 9,6 |
Patras | 17,9 | 10,0 | 10,6 | 12,5 | 15,6 | 20,1 | 24,1 | 26,4 | 26,7 | 23,5 | 19,0 | 14,5 | 11,4 |
Korfu | 17,5 | 9,7 | 10,3 | 12,0 | 14,9 | 19,6 | 23,9 | 26,4 | 26,3 | 22,7 | 18,4 | 14,3 | 11,1 |
Argostoli | 18,1 | 11,5 | 11,5 | 12,9 | 15,2 | 19,4 | 23,3 | 25,5 | 25,9 | 23,4 | 19,7 | 15,7 | 12,8 |
Chania | 18,5 | 11,6 | 11,8 | 13,2 | 16,3 | 20,1 | 24,5 | 26,5 | 26,1 | 23,3 | 19,4 | 16,1 | 13,1 |
Elefisina | 18,3 | 9,2 | 9,7 | 11,8 | 15,9 | 21,4 | 26,1 | 28,6 | 28,2 | 24,3 | 19,0 | 14,4 | 10,9 |
Heraklion | 18,7 | 12,1 | 12,2 | 13,5 | 16,5 | 20,3 | 24,4 | 26,1 | 26,0 | 23,5 | 20,0 | 16,6 | 13,7 |
Kalamata | 17,8 | 10,2 | 10,6 | 12,3 | 15,2 | 19,7 | 24,1 | 26,4 | 26,3 | 23,2 | 18,9 | 14,8 | 11,7 |
Tripoli | 14,1 | 5,1 | 5,8 | 7,9 | 11,7 | 17,0 | 22,0 | 24,5 | 24,1 | 20,0 | 14,6 | 10,1 | 6,7 |
Lamia | 16,5 | 7,1 | 8,0 | 10,5 | 14,8 | 20,1 | 25,3 | 26,9 | 25,9 | 22,4 | 16,9 | 11,8 | 8,3 |
Leminosi | 15,9 | 7,4 | 7,7 | 9,7 | 13,6 | 18,4 | 23,6 | 25,9 | 25,2 | 21,5 | 16,9 | 12,3 | 9,0 |
Nakisosi | 18,2 | 12,1 | 12,2 | 13,3 | 16,0 | 19,5 | 23,3 | 24,9 | 24,8 | 22,8 | 19,6 | 16,3 | 13,6 |
Filadelfeia ya sasa | 17,6 | 8,7 | 9,3 | 11,2 | 15,3 | 20,7 | 25,6 | 28,0 | 27,4 | 23,3 | 18,1 | 13,7 | 10,3 |
Rodesi | 19,1 | 11,9 | 12,1 | 13,6 | 16,6 | 20,5 | 24,7 | 26,9 | 27,1 | 24,6 | 20,8 | 16,5 | 13,4 |
Tatoi | 16,4 | 7,3 | 7,8 | 9,9 | 14,2 | 19,6 | 24,6 | 26,9 | 26,3 | 22,1 | 17,0 | 12,4 | 9,9 |
Atheni (Eliniko) | 18,5 | 10,3 | 10,6 | 12,3 | 15,9 | 20,7 | 25,2 | 28,0 | 27,8 | 24,2 | 19,5 | 15,4 | 12,0 |
Samosi | 18,4 | 10,3 | 10,0 | 12,1 | 15,9 | 20,6 | 25,5 | 28,4 | 27,9 | 24,3 | 19,4 | 14,5 | 11,9 |
Lerapetra | 19,7 | 12,9 | 12,9 | 14,2 | 17,0 | 20,9 | 25,4 | 27,8 | 27,7 | 24,9 | 21,0 | 17,5 | 14,5 |
Mytilini | 17,6 | 9,5 | 9,9 | 11,6 | 15,6 | 20,2 | 24,7 | 26,6 | 26,1 | 22,9 | 18,5 | 14,3 | 11,3 |
Kasitoria | 12,9 | 0,5 | 2,7 | 6,7 | 11,6 | 16,8 | 21,0 | 23,1 | 22,5 | 18,4 | 12,6 | 5,0 | 1,2 |
Grevena | 13,4 | 2,0 | 3,0 | 6,0 | 12,7 | 15,2 | 20,3 | 23,5 | 23,9 | 14,9 | 11,3 | 7,0 | 3,0 |
Piraeusi | 12,35 | 14,5 | 18,1 | 24,4 | 23,5 | 29,1 | 31,5 | 39,2 | 39,1 | 29,0 | 20,1 | 13,0 | 12,7 |
Oraiokastiro | 15,6 | 11,9 | 22,8 | 33,7 | 27,4 | 19,7 | 14,3 | 25,4 | 15,5 | 11,2 | 17,0 | 9,0 | 4,5 |