Kanisa la Kigiriki la Othodoksi ni fundisho linalowakilisha idadi kubwa ya watu nchini Ugiriki, na inatambulika kikatiba kama ‘dini inayofuatwa’ na taifa. Dini nyingine kubwa katika Ugiriki ni Ukatoliki, Uislamu na Uprotestanti.
Katiba ya Ugiriki katika sehemu II: mahusiano baina ya kanisa na serikali, Ibara 3 inataja:
Dini inayofuatwa katika Ugiriki ni ile ya kanisa la Kristu la Othodoksi la Kimashariki. Kanisa hilo la Ugiriki, likimtambua Yesu Kristo wetu kama kichwa chake, imefungamanishwa na fundisho la Kanisa Kuu la Kristo katika Konstantinopile na kwa kila Kanisa Lingine la Kristo lenye mafundisho sawa. Linashikilia bila kusita, kama wanavyofanya, utume mtakatifu, na mila za kidini, na inasimamiwa na Sinodi Mtakatifu wa Maaskofu wanaohudumu, na Mtakatifu Sinodi wa kudumu, likianzishwa na kujumuika kama ilivyoelekezwa katika Mkataba wa Kisheria wa Kanisa, chini ya masharti ya mfumodume wa Tome wa Juni 29, 1850, na Sheria ya Sinodi ya Mkataba wa Septemba 4, 1928.