Katika jamii ya Kigiriki, chakula huambatana na shughuli na hali nyingi. Mila za Kigiriki hupendekeza vyakula maalum wakati wa likizo, arusi, ubatizo, mazishi, au matukio ya kipekee katika jamii. Mapishi maalum ya kitamaduni huwa ni sehemu muhimu ya maadhimisho katika maeneo mengi ya Ugiriki. Wanawake wa jimbo la Ugiriki na wanachama wote wa jumuiya ndogo za mitaa hupitisha mapishi haya vizazi hata vizazi.
Vyakula maalum husheheni misimu ya Krisimasi, Mwaka Mpya na Pasaka, ingawa katika miaka ya karibuni vyakula vya kigeni vimechukua pahala pa vyakula hivi asili, hasa katika miji mikubwa. Wakristo wa Othodoksi hufunga kwa siku kadhaa za mwaka. Hii ina maana kuwa katika nyakati maalum (kabla ya siku kuu kubwa –Krisimasi, Pasaka, na Agosti 15) vyakula Fulani kama nyama, jibini, mayai au mafuta hutengwa. Mifungo inayopendekezwa na kanisa la kiothodoksi ni tabia nzuri za ulaji ambazo hudumisha afya nzuri na kuhimiza matumiza ya bidhaa za kilimo za kienyeji. Baaadhi ya mapishi ya kitamaduni hutuonyesha kuwa maendeleo yanaweza kupatikana kutokana na mboga, sawia na protini kutoka kwa wanyama, almradi aina mbalimbali za protini zitumike, kama vile kunde, nafaka, mikate, mchele, na kadhalika.
Katika Ugiriki, chakula maalum cha Krisimasi ni nyama ya nguruwe. Inashikilia nafasi maarufu katika mapishi yao kwani nyama ilikuwa jambo la ‘anasa’, na ililiwa katika hafla maalum. Wanyama wa familia walifugwa hasa kawa maziwa na mayai. Ulaji nyama, hata ilotibiwa, ilikuwa nadra kwa wengi. Badala yake, matajiri walizoea nyama ya kondoo, mbuzi, kuku, ndege, na michezo.
Kila eneo la Ugiriki lilikuza mapishi yake, kutegemea sifa maalum ya mazingira (kisiwani, milimani, mijini), malighafi zilizoko, lakini kwa mujibu wa sheria na tamaduni za kidini. Kwa mfano, katika Yuboea, mapishi yao ya Krisimasi yaliitwa ‘Babesi’. Ni matumbo yaliyochemshwa, na kutiwa ini, wengu, na viungo. Rangi ya wengu ilikuwa na ishara: ikiwa safi iliashiria wema, ikiwa manjano iliashiria maafa. Katika Epirusi (Zagorochoria), walitengeneza “sipagana” (aina ya keki), zilizoashiria uchanga wa Krito horini. Dodekanesi hujivunia ‘jiapurakia’, iliyotiwa majani ya kabichi, mchele na nyama ya kusaga. Majani ya kabichi kufungia nyama ya kusaga kuliashiria mavazi ya Kristo ya utotoni. Katika Thurasi kulikuwa na aina tisa tofauti za vyakula vilivyopakuliwa mezani, vibichi, na vilivyofaa wakati wa kufunga. Mfano wake hapa ulihusiana na nia ya wingi wa chakula kwa watu wote mwaka mzima. Aidha, desturi moja ya Krisimasi katika mikoa yote ya Ugiriki ni keki ya Krisimasi inayopambwa kwa mapambo tofauti yanayoashiria nguvu za Mungu. Kristosomo, mkate uliopambwa kwa msalaba hutandazwa mezani siku ya Krisimasi. Daima hutengenezwa kwa vifaa bora zaidi (unga ngano, njugu, ufuta, na viungo. Ikiangukia upande wa nyuma, mwaka utakuwa mbaya, na ikiangukia upande wa juu, mwaka utakwenda vizuri.
Kitindamlo hakikosi katika meza ya vyakula vya Wagiriki. Kitindamlo cha kawaida ni panikeki kwa asali na divai, ambapo asali iliashiria wingi wa bidhaa mwaka woter, na divai ikiashiria ukuaji na kuenea kwa familia kama mzabibu. Hatimaye, matunda kama vile makomamanga na tufaha daima zilikuwa mezani, ili familia iwe na rangi ‘akiki’ ya afya. Tamtamu nyinginezo ni ‘kourampiedesi’ (biskuti za sukari nyingi), ‘madipo’ (kwa asali), ‘melomakarona’ (kwa asali na njugu), ‘tiganopisoma’ (kwa jibini), ‘serotigana’ na kijiko cha tamtamu (matunda kama vile cheri chungu, zabibu, ndimu, bagamoti, zilizopikwa kwa sukari.
TKeki inayotayarishwa kwa ujio wa Mwaka Mpya huwa na ‘sarafu ya dhahabu’, ambayo kulingana na mila, huleta heri njema kwa yule aipataye. Wakati wa Epifania, Ubatizo wa Kristu husherehekewa, na maji hutakaswa kwa kuurusha msalaba ndani yake. Wengi hupiga mbizi ili ‘kuushika’ msalaba, unaoaminika kuleta si tu bahati, bali pia ulinzi dhidi ya maovu na mateso.
Siku hizi, nyumba hurembeshwa wakati wa Krisimasi na Mwaka Mpya kwa mapambo mbalimbali ya msimu wa sherehe, na mti wa Krisimasi hutawala mandhari, japo desturi hii ilifika Ugiriki kutoka mataifa ya kaskazini. Kitamaduni, Wagiriki walipamba nyumba zao na mashua ya Krisimasi, iliyoonyesha umuhimu wa bahari katika maisha yao.
Ugiriki hasa ilikuwa nchi ya kilimo na shughuli zinazohusihwa na kilimo ni bayana katika desturi za kidini za Kigiriki. Kuwashwa kwa moto wakati wa baridi, kukihusishwa na matarajio ya mazao, ni kiini cha marejeleo.
Katika eneo lolote la Ugiriki, Pasaka ina tabia za asili na hisia za kipekee. Ina maadili yake yenyewe, muhuri binafsi, na aina ambazo zimekita mizizi katika mila za jadi. Katika mila za kisasa za Kigiriki za Pasaka, chakula cha jioni huwa ni pamoja na “mageiritisa” (aina ya supu ya mnyama na mboga) kama chakula kikuu, kinacholiwa jioni ya Ufufuko baada ya Litajia ya Ufufuko kanisani, kuvunjwa kwa mayai mekundu (yakiashiria damu ya Kristu), ‘busu la upendo’ wakati wa ufufuko na kuchomwa kwa mwanakondoo siku ya Jumapili ya Pasaka. Vitumbua vyenye viungo maalum na ladha tele pia hutengenezwa, pamoja na ‘tisourekia’ (aina ya mkate mtamu wenye mastiki na machilepi).
Mastiki ni resini ya kunukia itokanayo na mti wa mastiki unaokua tu katika Chiosi (kisiwa kilicho Mashariki mwa Eegeni). Tangu zamani, mastiki imekuwa na matumizi mengi: kuongeza vyakula na keki ladha tamu, kutengenezea samani na vyombo vya muziki, na uundaji wa dawa.