Mfumo wa Utawala
Jiografia, Habari ya Idadi ya Watu
Mila, Tamaduni

Sera za uhamiaji

Afya, Kazi, Elimu

Huduma, Taasisi, Ushauri
Uko hapa:  Sera za uhamiaji / Uraia – kufanywa kuwa raia

Uraia – kufanywa kuwa raia

Ιθαγένεια-Πολιτογράφηση

Maneno ‘Uraia wa Kigiriki’ yanamaanisha nini?

Uraia wa Kigiriki ni uhusiano wa kisheria kati ya mtu na serikali.

kufanywa kuwa raia kunamaanisha nini?

Kufanywa kuwa raia ni hali ya kupokea uraia wan chi ya kigeni (watu wanaotoka nje ya mipaka ya Ugiriki) na wageni wenye asili ya Kigiriki (raia wa nchi zingine).

Ni kwa njia gani naweza kupata uraia wa Kigiriki?

➢ Kwa kuzaliwa

  1. Mtoto wa wazazi wa Kigiriki hupata uraia wa Ugiriki kwa kuzaliwa.
  2. Uraia wa Ugiriki hupatikana kufuatia kuzaliwa kwa mtoto nchini Ugiriki iwapo:

    • a. mmoja wa wazazi alizaliwa Ugiriki na ni mkaazi wa kudumu katika nchi ya kuzaliwa

      b. mtoto hatachukua uraia wa nchi nyingine kwa kuzaliwa, ama kwa vyovyote kufuatia tamko la wazazi wake kwa mamlaka za kigeni, iwapo sheria ya uraia wa wazazi inahitaji kutolewa kwa tamko kama hilo

      c. uraia wake hujulikani. Hata hivyo, kutoweza kutambua uraia wa kigeni unaoweza kupatikana wakati wa kuzaliwa, sio kwa kukataa kwa wazazi kushirikiana.

Ikumbukwe kwamba wakati aya hii imeandikwa, Kigiriki Uraia Kanuni ni kuwekwa chini ya online ushauri wa umma mpaka 25.05.15, kuboresha masharti yake.

Je, mama au baba (asiye katika ndoa) anaweza kumwombea mtoto wake uraia wa Kigiriki (kama ilivyoelezwa hapo juu)?

Ndio!

➢ Kwa kutambuliwa

  • Mtoto wa kigeni aliyezaliwa nje ya ndoa, na anatambulika kisheria na raia wa Ugiriki kwa kupenda au kutambuliwa rasmi na mahakama, huwa raia wa Ugiriki iwapo wakati wa kutambuliwa huyo mtoto wa kigeni alikuwa chini ya umri wa miaka 18.
➢ Kwa kutwaliwa
  • Mtu aliyetwaliwa na raia wa Ugiriki utotoni huwa Mgiriki kutoka siku ya kutwaliwa kwake.
➢ Kwa Kufanywa kuwa raian

Mchakato wa kufanywa kuwa raia ni upi?

Tawala za Mashinani za kila Manispaa huwajibika katika jambo hili. Maombi ya kufanywa kuwa raia hutumwa kwa idara husika kutegemea Manispaa unayoishi. Katika jedwali lifuatalo utaona hatua zote zinazohitajika katika mchakato wa kufanywa kuwa raia. Jedwali lenye mchakato wa kufanywa kuwa raia kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani laweza kupatikana : hapa

Hapa chini unaweza kuona kwa kina maelezo 7 kutoka kwa Tawala Mashinani za Atika

STEP 1. Hati ambatani

  • Picha 1
  • Tamko la kufanywa kuwa raia. Hufanyika katika Manispaa ya Makazi, wakiwemo mashahidi 2 wa Kigiriki
  • Nakala halisi ya pasi halali ya kusafiria na kurasa zake zote. Pia, nakala ya pasi zote za zamani za kusafiria na tamko la dhati la kufika na kutoka kwote nchini tangu 2005 hadi sasa.
  • Nakala halisi ya kibali halali cha makazi. (nambari ya cheti)
  • MAAMUZI tangulizi au VYETI kwa VIBALI VYOTE VYA MAKAZI walau kuanzia Machi 24, 2005 hadi sasa. Kwa raia wa taifa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, wenzi wa ndoa wa Wagiriki walio na mtoto, wakimbizi wa kisiasa wanaotambulika, na watu wasio na taifa, vibali mtawalia vya makazi kwa miaka mitatu tangu siku ya kutuma ombi bila nyaraka toshelezi. Wenzi wa ndoa wa raia wa Ugiriki wasio na watoto hawajumuishwi, na miaka saba ya makazi halali tangu siku ya kutuma maombi inahitajika.
  • Cheti HALISI cha kuzaliwa katika LUGHA YA KIGENI – na cheti cha kuolewa kwa wanawake – kilichothibitishwa kulingana na taifa la asili na kisha kutafsiriwa na Idara ya Kutafsiri ya Wizara ya Mambo ya Kigeni (10 Mt. ARIONOSI, Atheni) au na wakili wa Ugiriki (hakuna vituao vya kutafsiri).
  • Ada ya kusimamia (NAKALA YA TUPE, KAE 3744) na mamlaka ya ushuru: Yuoro 700 chini ya jina la anayeomba.
  • Nakala ya Nambari ya Malipo ya Uzeeni (AMKA)
  • Nakala za ilani za tathmini za ushuru za hivi karibuni, pamoja na za miaka 7 (saba) iliyopita.
  • Iwapo zinapatikana: Hati za Malipo ya Uzeeni (k.m IKA, OAEE), na cheti cha makazi

HATUA 2: Jaza ombi la Kufanywa kuwa raia

(sehemu zote ni lazima kujazwa)
Ombi la Kufanywa kuwa Raia

HATUA 3: Fanya miadi ya kuwasilisha maombi na hati andamani

Baada ya kuwasilisha nyaraka kwenye tarehe ans muda uliowekewa na iwapo hakuna kilichoachwa, taratibu zinazofuatwa kukamilisha uraia wako zinazingatiwa bila kuhitaji jambo lingine lolote kutoka kwako. Iwapo utahitajika kuongeza hati andamani, Huduma yetu itakuandikia barua. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kuifahamisha Huduma yetu kuhsusu mabadiliko yoyote ya makazi yako, kwa kutuma tamko la dhati kuhusu mabadiliko hayo pamoja na hati andamani, na kuzituma kwa Ukatibu wa Huduma yetu (6 Mt. Ipatiasi, Jumatatu hadi Ijumaa, 8:00-14-30). Hatimaye, tukumbuke kwamba habari inayohitajika kutoka kwako inahusu kufanywa upya kwa kibali cha makazi, na nakala yake itumwe kwa Huduma yetu punde itolewapo.

Kwa Waatheni: Ili kuweka miadi, unastahili kufika katika huduma yetu, 6 Mt. Ipatiasi, Atheni, Orofa ya Kwanza, Ofisi 1, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa: 8:00-14:00, 6 Mt. Ipatiasi, Atheni, Ofisi 1. Mawakili hupatikana siku yoyote ya kazi (Jumatatu hadi Ijumaa).

HATUA 4: Mahojiano na Kamati Maalum ya Kufanywa kuwa Raia

Miezi sita baada ya kutuma ombi la kupata uraia wa Ugiriki kwa njia ya kufanywa kuwa raia, utaulizwa kufanya mahojiano na kamati husika chini ya Tawala za Mashinani unakoishi.

Lengo la hiyo kamati ni nini?
Kutathmini mahitaji muhimu ya kufanywa kuwa raia yametimizwa.

Mahojiano huchukua muda gani?
Takribani dakika 20-25.

Maswali huwa kuhusu nini?
Maswali ya kwanza huhusu maisha yako, kazi yako, mahali ulikotoka. Kisha huhusu historia ya Ugiriki, jiografia, siasa, unakoishi, na mambo ibuka ambayo ni muhimu kwa jamii ya Ugiriki.

Mifano ya maswali katika kila mada:

Historia

  • Ni sikukuu gani unazojua? Au ni nini husherehekewa Oktoba 28 na Machi 25?
  • Unafahamu nini kuhusu mapinduzi ya Ugiriki?
  • ‘Filiki Eteria’ ilikuwa nini?
  • Unajua nini kuhusu kifungu ‘krifo scholio’??
  • Taja mashujaa/watu mashuhuri katika Mapinduzi ya Ugiriki
  • Unajua nini kuhusu 1. Metasasi?
  • Unajua nini kuhusu mkasa wa Asia ya Chini?
  • Umewahi kusikia kuhusu ‘Alekisanda Mkuu’, una lipi la kutuambia kumhusu?
  • Unajua nini kuhusu Homeri?
  • Mada ya Odisei na Iliadi inahusu nini?
  • Anguko la Konstantinopile lilikuwa lini? 
  • Ni nani aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Ugiriki? Au ni mji gani ulikuwa Mji Mkuu wa kwanza wa Ugiriki?

Jiografia

  • Ni visiwa gani vikubwa zaidi vya Ugiriki?
  • Taja mataifa yanayopakana na Ugiriki.
  • Je, unafahamu mahali Ugiriki inapatikana katika ramani ya Ulaya?
  • Mipaka ya bahari na ardhi ya Ugiriki ni gani?
  • Ni bahari gani zinazozunguka taifa letu?
  • Unaweza kutaja visiwa vya Epitanese?
  • Ni safu gani tena ya visiwa unayojua?
  • Sailadesi walipata jina lao kutoka wapi?
  • Je, unafahamu baadhi ya visiwa vikubwa zaidi vya Ugiriki?
  • Unaweza kutaja baadhi ya mito inayofahamika vyema nchini Ugiriki?
  • Taja baadhi ya maziwa, asili au bandia.
  • Ni miji gani mikubwa nchini unayofahamu?

Tamaduni

  • Unafahamu mji wa Olimpia ulipataje jina lake?
  • Umewahi kuzuru Kinososi na Faisitosi? Unajua chochote kuhusu sanamu hizi?
  • Unafahamu nini kuhus Epidaurusi?
  • Marumaru ya Eligini ni nini yalipata jina lake wapi?
  • Umewahi kutembelea Parithenoni, na una lolote la unafahamu unaweza kutuambia?
  • Megaro Mousikisi ni nini?
  • Unajua nini kuhusu Akiropolisi?
  • Unaweza kutaja washairi na waandishi muhimu zaidi wa Ugiriki?
  • Umewahi kutembelea makavazi? Unajua baadhi ya makavazi?
  • Unajua wasanii wa Kigiriki? Umewahi kutembelea ukumbi wa sanaa wa kitaifa? Ni maonyesho gani hupatikana?
  • Unajua nini kuhusu sifa za Wachazidaki au Watheodoraki?
  • Unawafahamu wanamuziki au watunzi?

Siasa

  • Rais wa Jamhuri ya Helenika ni nani?
  • Waziri Mkuu wa Ugiriki, au Waziri wa Fedha ni nani?
  • Kuna wajumbe wangapi katika Bunge la Kitaifa?
  • Mahakama kuu ni zipi au unafahamu nini kuhusu Areiosi Pagosi?
  • Unaijua katiba?
  • Ugiriki ilijiunga na Umoja wa Ulaya lini?
  • Baraza la Ulaya ni nini?
  • Unajua nini kuhusu Umoja wa Mataifa?

Maisha ya kawaida nchini

  • Ni magazeti gani huchapishwa katika wilaya yako?
  • Taja miraba mikubwa zaidi katika wilaya yako.
  • Meya wa mji wako unaoishi ni nani?
  • Taja baadhi ya pwani za wilaya yako (iwapo zipo k.m iwapo mtu anaishi Lefikada, Milosi)

Maswala ibuka

  • IMF (Hazina ya Kimataifa ya Fedha) inasimamia nini?
  • Mkataba ni nini?
  • Unajua nini kuhusu Troika?

Majibu mengi yanaweza kupatika katika kitabu “Greece, second home”3, wkinachofaa kusomwa na kila mtu mwenye nia ya ufahamu wa mchakato wa uraia.

Ikumbukwe kuwa katika busara ya Tume na mchakato wa uorodheshaji wa Kamati, uamuzi chanya au hasi huafikiwa na Kamati, na kuwasilishwa kwa hati ya Huduma. Iwapo kuna uamuzi hasi wa Kamati, pingamizi inaweza kuwasilishwa kwa Baraza la Uraia la Wizara ya Mambo ya Ndani, katika kipindi cha siku 15 za kufahamishwa huo uamuzi. Katika busara ya Baraza la Uraia, pingamizi inaweza kukubaliwa au kutupiliwa mbali.

A. Baada ya hapo, kuna uamuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, ambao huambatana na makubaliano ya ombi la uraia wa Ugiriki, na kufuatiwa na tangazo la uraia kwa huduma, ili mhusika aalikwe kula kiapo kama ilivyoelezewa katika hatua ya 6 hapa chini.

B. Ombi linakataliwa na uamuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani na ombi jipya laweza kutumwa kwa ada ya usimamizi iliyopunguzwa (Yuro 200) baada ya mwaka mmoja kutoka siku ya uamuzi hasi wa Waziri.


3: This manual is offered as an aid (electronic) for foreigners interested in acquiring the Greek citizenship by naturalization, by the Ministry of Interior and Administrative Reconstruction. The particular book contains concise information about Greek history, culture, geography, etc. However the manual was written with the previous legislation and its content does not touch on all the issues that may be mentioned during the interview. Therefore it would be desirable to use other sources of information. As http://www.metanastes.gr/ithagenia-omogenia/politografisi-alladopou/209-sinentefksi.html

HATUA 5: Kutolewa kua uamuzi wa kupatiana uraia wa Ugiriki

Kufuatia tathimini chanya ya Kamati na kuwasilishwa kwa uamuzi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ili uamuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ufuatie. Baada ya kuchapishwa kwa muhtasari wa uamuzi huo wa uraia katika Gazeti la Serikali na ilani kutolewa kwa hudma, kinachofuatia ni kula kiapo.

HATUA 6: Kiapo cha Raia wa Ugiriki

Mchakato wa uraia hukamilika kwa kiapo cha raia wa Ugiriki, na Huduma kutuma barua na maelezo ya tarehe na saa ya kula kiapo. Pamoja na barua hii tamko la dhati hutumwa ambapo maelezo ya watoto yametajwa.

HATUA 7: Mamlaka ya usajili wa umma au/na uandikishaji katika Sajili ya Wanaume wa Manispaa ya Atheni*

Ni hatua ya mwisho inayohusisha Huduma baada ya kula kiapo, na inahusiana na mamlaka waliyonayo wanawake kwa kusajiliwa kwao katika Manispaa ya Mji wa Atheni, huku uamuzi wa kuwasajili wanaume katika Sajili ya Wanaume ya Mji wa Atheni unahitajika kwanza na kisha wajiandikishe katika sajili ya Manispaa.

* Ikumbukwe kuwa watoto wa Wagiriki waliofanywa kuwa raia hupata uraia wa Ugiriki, almuradi hawajahitimu miaka 18, na hawakuwa wameoa au kuolewa wakati wa kiapo cha wazazi wao. Iwapo una haja na mchakato huu unapaswa kuwasiliana na Manispaa ya Atheni. Ikiwa watoto ni watu wazima kufikia wakati wa kiapo, basi wanahitajika kuwasilisha ombi upya.

CAN I? Kitambulisho cha Kitaifa cha Ugiriki Kibali cha Makazi cha Kazi Tegemezi (Miaka 2+kufanywa upya kwa miaka3) Kibali cha Makazi cha Miaka 10 Kibali cha Makazi ya Muda Mrefu – Kipindi cha Miaka 5 (Ulaya) Residence Permit of Greek family member or citizen of the EU Kibali cha Kizazi cha Pili Kibali cha Hakuna Makazi Bila Utaifa (Mtoto aliyezaliwa katika Ugiriki, hakuna uraia unaotambuliwa)
Sajiliwa katika Chuo Kikuu?√ x √ √ √ √ x x
Safiri ng’ambo?√ √ √ √ √ √ x x
Somea katika taifa la Shenjeni? √ x x √ √ (iwapo tu niko katika nchi sawa na yule aliyenisaidia kupata kibali.)** √ x x
Fanya kazi katika Umoja wa Ulaya? √ x X √ (* ni katika eneo la Shenjeni tu & na iwapo tu unaweza kupata kibali cha kazi katika nchi ambayo ningependa kufanya kazi)* √ **(iwapo tu niko katika nchi sawa na yule aliyenisaidia kupata kibali.) x x x
Kuwa na uhuru katika kutafuta kazi? √ x x x x x x x
Pata bima?√ √ √ √ √ √ x x
Fanya kazi katika sekta ya umma? √ x x x x x x x
Una haki za kisiasa?√ x x x x x x x
Fukuzwa Ugiriki?x x x x x x √ x
* ni katika eneo la Shenjeni tu & na iwapo tu unaweza kupata kibali cha kazi katika nchi ambayo ningependa kufanya kazi
** wapo tu niko katika nchi sawa na yule aliyenisaidia kupata kibali.

Rudi
Mradi wa 1.4.b/13 ‘Matangazo ya Redio ya masuala kuhusiana na wahamiaji, uzazi, na usambazaji mpana wa vifaa vilivyochapishwa, vya sauti na vielelezo’ ulifadhiliwa 95% na Hazina ya Jumuiya na 5% na Rasilimali za Kitaifa