Ndio! Iwapo wewe ni raia wa mataifa ya tatu na unaishi nchini na stakabadhi hitajika, uko huru kusafiri na kuishi popote utakapo nchini.
Ndio! Iwapo wewe ni raia wa mataifa ya tatu na unaishi nchini na stakabadhi hitajika, unaweza kuchukua bima (kulingana na hali yako ya kitaaluma) katika mashirika faafu ya bima. Una haki sawa za bima kama raia wa Ugiriki.
Hapana! Iwapo wewe ni raia wa mataifa ya tatu na unaishi nchini na stakabadhi hitajika, una haki ya kupata matibabu ya bure katika mashirika ya umma ya Mfumo wa Afya wa Kitaifa (ESY), kama raia wa Ugiriki. Utapata habari zaidi katika sura ya afya.
Ndio! Ukiingia katika taasisi, una haki ya kujulishwa sheria zake, sawia na haki na wajibu wako. Mawasiliano yako yafaa kuelekezwa na mwanadiplomasia au maafisa wa ubalozi wa nchi, na ambayo wewe ni raia au ulitoka, pamoja na mawakili wako.
Iwapo unaishi Ugiriki umejumuishwa katika masomo ya lazima, kama raia wa Ugiriki. Watoto wa chini wa miaka 18, wanaoshiriki viwango vyote vya elimu, wana uhuru wa kushiriki shughuli zote shuleni au katika jumuiya ya elimu. Haki ya elimu kwa watoto wa kigeni walio chini ya miaka 18 haina mjadala.(Imehakikishwa na Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Mtoto (Ibara ya 28) na sheria ya Kigiriki katika Katiba ya Ugiriki (Ibara 16 & 21) na katika nyaraka mbalimbali kama 73025/C2/2010. Habari zaidi ni katika sura ya Elimu).
Ili kumsajili mtoto wa chini ya miaka 18 katika shule za Kigiriki katika ngazi zote, stakabadhi muhimu zinazotolewa kwa raia wa Ugiriki zinahitajika.
Hata hivyo! Watoto (raia wa nchi za tatu) wanaweza kujiunga na shule za umma iwapo hawana stakabadhi za kutosha, iwapo: a) Wanalindwa na Serikali ya Ugiriki chini ya ulinzi wa kimataifa, na walio chini ya ulinzi wa Ubalozi wa Umoja wa Mataifa, b) Wametoka maeneo ambayo hali si tulivu, c) Wametuma ombi la ulinzi wa kimataifa d) Ni raia wa mataifa ya 3 wanaoishi Ugiriki, hata iwe uhalali wa makazi yao bado hujathibitishwa. (Habari zaidi katika sura ya Elimu).
Ndio!Ikiwa una elimu ya sekondari nchini Ugiriki nawe ni raia wa mataifa ya tatu, unaweza kupata elimu ya juu chini ya masharti yale yale ya raia wa Ugiriki (kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyoko).
Katika kukaa kwako nchini Ugiriki, lazima ufahamishe mamlaka ya Utawala wa Mashinani nchini, au Wakurugenzi wa Sera za Uhamaji katika Wizara ya Mambo ya Ndani:
Kwa masikitiko, iwapo una kibali cha makazi, lazima uondoke bila taarifa zaidi, kabla ya siku ya mwisho ya kumalizika kwa kibali chako, isipokuwa tu kama kabla ya kumalizika kwa muda huo uwe umetuma ombi la kufanya upya, na uwe umepata kibali cha aya ya 7 ya Ibara ya 8 na aya ya 5 ya ibara ya 9 ya Kanuni za Uhamaji L.4251/2014.
Kumbuka: Unaweza kupata orodha ya mashirika yanayotoa msaada wa kisheria katika sura ya mwisho.