THazina za bima katika Ugiriki9, zinazohusiana na taaluma za kawaida kabisa miongoni mwa raia wa mataifa ya tatu ni:
ΙΚΑ / ΕΤΑΜ | www.ika.gr |
ΟΑΕΕ (iliyokuwa TEBE) | www.oaee.gr |
OGA | www.oga.gr |
- Iwapo ungetaka kusajiliwa katika I.K.A.-E.T.A.M (jiandikishe katika sajili ya wanachama ya IKA) utahitaji vitu vifuatavyo:
Kwa sababu una bima ya IKA unaweza kutoa kijitabu cha afya. Kijitabu cha afya cha kibinafsi ndicho kitambulisho cha faida za bima na hela kwa aliyekatiwa bima. Kijitabu cha afya cha familia hutolewa kwa watu wa familia yako. https://www.ika.gr/gr/infopages/asf/insurance/bibhygine.cfm
Watu wafuatao wana hakai ya kupata kijitabu cha afya cha kibinafsi:
Idadi ya siku zinazohitajika yaweza kubadilika, na kwa hivyo yafaa upate habari kutoka ofisi za IKA au kwenye tovuti (tazama hapa chini, “Je, nina Bima?” Masharti yale yale yanatumika kwa kuongeza muda wa kijitabu cha afya ya kibinafsi: Nyaraka ambatani:
Ni hakika kwa familia ya aliyechukua bima ama uzeeni au ulemavu (mwenzi wa ndoa, mama, baba, watoto ambao hawajaolewa). Watoto huacha kuhesabiwa kuwa tegemezi wanapohitimu miaka 18. Sharit hili laweza kusongezwa iwapo hawana ajira au ni wanafunzi au kwa miaka 2 ya kukosa ajira baada ya kukamilisha masomo na wangali wanamtegemea mwenye bima kifedha.
Kwa vyovyote vile, watoto wanaweza kusimamiwa na bima ya wazazi wao hadi umri wa miaka 26. Stakabadhi ambatani:
Stakabadhi ambatani zinazohitajika katika usajili kwa Shirika la Bima ya Kijamii ya Wataalam Kujitegemea (OAEE) hubadilika kutegemea taaluma ya mtu. Unaweza kupata maelezo ya kina katika tovuti http://www.oaee.gr/asfalish.asp?catasf_id=189&banner_pgc=11.
Maagizo ya Kijumla kwa stakabadhi ambatani:
Tafadhali fahamu kwamba:
Kwa wale walio na haki ya kupata bima kutoka OAEE na kijitabu cha afya, masharti ni sawa na Kijitabu cha Kibinafsi na cha Familia cha IKA. Stakabadhi ambatani:
Stakabadhi ambatani zinazohitajika kwa usajili katika OGA kama mtu aliyejiajiri (unapewa bima kwa kujiwajibikia na Tawi Kuu la Bima la OGA 11) na ujilipie michango ya bima:
Nchini Ugiriki, kila mwajiriwa ana haki fulani kama ilivyo kote katika Umoja wa Ulaya
Kila taifa la Umoja wa Ulaya lazima lihakikishe sheria zake za kitaifa zinalinda sheria za Umoja wa Ulaya. Taifa la Ugiriki limehukumiwa mara kadhaa kwa kukiuka ama kushindwa kulinda haki za kazi. http://ec.europa.eu/social/main.jsp?catId=82&langId=el
Mfumo wa bima ya kijamii nchini Ugiriki ni mojawapo ya mbinu za kusambaza mapato na mshikamano wa kijamii miongoni mwa walioajiriwa katika taasisi, wasio na ajira, wazee, na wenye kuhitaji ulinzi wa kijamii. Kazi za kimsingi za mashirika ya bima ni:
Fedha za bima ya kijamii hutolewa katika bajeti ya serikali na michango ya waajiri na waajiriwa. Michango hiyo ni ya lazima, hata iwe mwajiriwa ana mpango wa bima na shirika lingine (la kigeni ama la kibinafsi).
Ili kujua iwapo umewekewa bima au la (kuangalia uwezo wako wa bima, unaweza kutumia jukwaa la tovuti), tazama hapa chini. Unaweza pia kutembelea tawi la shirika la bima unakosajiliwa, japo wanashauri matumizi ya huduma za kieletroniki ili kuzuia misongamano katika matawi yao, na wewe kubaguliwa kwa vyovyote na mfanyikazi wao.
Mfumo wa ‘ATLAS’ hukusanya habari za watu wote wenye bima (tawasifu ya bima) kutoka kwa mashirika ya bima na zinaweza kupatikana katika tovuti https://www.atlas.gov.gr. Kwa upande wa OGA, uanweza kupata habari sahihi zaidi kwa kutembelea tawi lao katika eneo ulikosajiliwa. Kwa upande wa IKA na OAEE, unaweza kurejelea majukwaa ya kielektroniki tovuti kupitia anwani hizi:
*Tafadhali kumbuka kuwa: Ili kutumia huduma za tovuti, utahitajika kwanza kuwa na akaunti yako ya kibinafsi katika ‘taxisnet’ upate ‘jina la mtumiaji’ na ‘nenosiri’
Katika muktadha wa mabadiliko ya karibuni katika utenda kazi wa mfumo wa bima ya kijamii, kila hazina ya bima inawajibika kwa pensheni za walio na bima, lakini huduma za afya za hazina nyingi ziliunganishwa katika Shirika la Kitaifa la Utoaji Huduma za Afya (EOPYY).
EOPYY hushirikiana na muungano wa vituo vya afya kote nchini na muungano wa madaktari mahsusi katika huduma za afya ya msingi (angalia sura kuhusu ‘afya) Kuhusu maswala ya afya ya sekondari (hospitali), walio na bima sharti waonyeshe kijitabu cha afya wakati wa kulazwa hospitalini, ambacho hutolewa na kuapudetiwa na kila shirika la bima kwa niaba yao na familia yao.
Inategemea! Kila hazina ya bima ina masharti yake. Pensheni hutolewa kwa sababu ya uzee, kifo cha mwenzi wa ndoa, au ulemavu. Wale ambao wamekamilisha kiwango fulani cha siku za kufanya kazi (stempu za bima) na kufikia kiwango fulani cha umri, wanaweza kupata malipo ya uzeeni. Vikwazo vya miaka hutofautiana kati ya wanaume na wanawake, na siku za bima hutofautiana kutegemea kazi unayofanya.
Makundi maalum ya kazi ni yaliyoorodheshwa kama nzito na yenye madhara ya kiafya (kama vile wafanyakazi wa mjengo, waajiriwa wa melini, n.k), ambapo waajiriwa hustaafu mapema. Orodha husika ya hizi kazi hurudiwa mara kwa mara, na ni vyema kwako kuwasiliana na hazina yako ya bima kupata ushauri zaidi.
Shirika linalopokea malalamishi kuhusu ukiukwaji wa haki za kazi ni Askari Wakaguzi wa Leba (SEPE) chini ya Wizara ya Leba, Bima ya Jamii na Maslahi. Ofisi zake ziko Atheni (10 Mt. Agisilaou, P.C. 10437, Tel. 2105289281), lakini unaweza kupata matawi yake kote nchini. Unaweza kupata orodha kamili ya anwani na maelezo ya mawasiliano ya SEPE katika tovuti 12.
TMashirika yanayotoa huduma za ushauri wa kisheria kuhusu masuala ya kazi ni:
Hapana!
Hapana, labda iwe umewasiliana na tawi lenye mamlaka kuwasilisha malalamishi yako, (Tangazo la kutokubaliana kuhus deta ya bima – Malalamishi). ‘Ombudsman’ ya Ugiriki, ikiwajibika kudhibiti hazina zote za bima, yaweza kuingilia tu ikiwa IKA itachelewa kuchunguza malalamishi yako ama iwe imefanya uamuzi unaouchukulia kuwa kinyume cha sheria.