Mfumo wa Utawala
Jiografia, Habari ya Idadi ya Watu
Mila, Tamaduni

Sera za uhamiaji

Afya, Kazi, Elimu

Huduma, Taasisi, Ushauri
Uko hapa:  Afya, Kazi, Elimu / UKOSEFU WA AJIRA

UKOSEFU WA AJIRA

Ανεργία

Nilipoteza kazi yangu. Nifanyeje?

Iwapo hujaajiirwa, unaweza kuwasiliana na Shirika la Kuwezesha Ajira (OAED) tambalo litakuwezesha kupata bima, upate faida za waso ajira kwa kipindi fulani cha wakati, ushiriki mafunzo ya kiufunzi na kupata ushauri wa kupata kazi (huduma za ushauri wa ajira).

Kwa nini nijisajilishe katika OEAD? Wanatoa huduma gani?

OAED huendesha shughuli zake kwa misingi ya nguzo zifuatazo:

  • kuinuliwa kupata ajira
  • bima kwa wasio na ajira
  • hifadhi ya wajawazito na familia
  • - Elimu ya ufundi na mafunzo
OAED hutoa bima kwa muda mfupi kwa waliosajiliwa wasio na ajira, kutegemea muda wao wa kazi na kutokuwa na ajira. Zaidi ya hapo, OAED hutoa faida za kutokuwa na ajira kwa kipindi fulani cha wakati kwa watu walopoteza kazi yao kufuatia kukamilika kwa kandarasi zao au kuachishwa kazi. Hatimaye, shirika hili hutoa faida nyinginezo (huduma na pesa) kama marupurupu za familia, marupurupu za uja uzito, au kwa akina mama wanaofanya kazi (hapo awali wangewaandikisha watoto wao kwa Shirika la Hazina ya Wafanyikazi).

OEAD pia hutoa huduma za ushauri wa ajira,ambapo watu wenye haja hupata ushauri wa jinsi ya kupenya katika soko la ajira (tazama sura kuhusu ‘Huduma za Ushauri wa Ajira’ hapa chini).

Shirika hili limetekeleza taasisi ya mafunzo katika Shule 51 za Elimu ya Kiufundi kwa wanafunzi wasio na ajira, ambapo hufunza makundi mbalimbali na kuyaajiir kama makurutu kwa muda mfupi katika biashara husika, na kuwapa marupurupu na bima ya OAED.

Ukuzaji wa sera za ajira hujumuisha kupunguzwa kwa gharama za leba kwa wanabiashara, kwa kumarupurupu mishahara na matoleo ya bima ya kijamii, iwapo biashara hiyo itamwajiri mtu ambaye amesajiliwa katika OAED na ni mmoja wa wale wameathiriwa kabisa na ukosefu wa ajira na yuko katika mazingira magumu.

Unaweza kupata habari zaidi kuhusu Shirika la Kuwezesha Ajira katika tovuti yao rasmi www.oaed.gr.

Unaweza kupata habari kuhusu mipangilio ya Ushauri wa Ajira katika matawi yote ya Shirika (ni muhimu kushirikiana na mshauri wa ajira), na pia katika:

    OAED – Kituo cha Maelekezi bora ya Kiufundi
      Anwani: 52 Mt. Piraeusi., Atheni
      Tel.: 2105247479, 2105288445
      Barua pepe: pkep@oaed.gr
    OAED – Ukurugenzi wa Maelekezi ya Kiufundi (Α1)
      Anwani: 2 Mt. Gounari & 518 Mt. Vouliagimeni, Atheni
      Tel.: 2109989629, 2109989634.
      Barua pepe: a1@oaed.gr
    OAED – Ukurugenzi wa Kuratibu Maendeleo ya Huduma za Ajira
      Anwani: 8 Mt. Ethinikisi Antistaseo, Alimosi
      Tel: 2109989184, 2109989173
      Barua pepe: symvouleftiki@oaed.gr

Utaratibu wa kujisajilisha katika OAED ni gani?

Ili kusajili katika OAED na kupokea kadi ya kutokuwa na kazi, utahitaji kutuma stakabadhi zifuatazo kwa ofisi ya Shirika iliyo karibu na wewe:

  • Pasi halali ya usafiri au kitambulisho
  • Kibali cha makazi au kibali cha makazi (kwa raia wa mataifa ya tatu
  • Ilani ya mapato na ushuru ya karibuni zaidi, au isipokuwepo, nakala ya fomu ya ushuru iliyokwisha kujazwa tayari (E1). Watu wasio na ajira na wanatemea wengine (k.v watoto) wanahitaji fomu za wazazi wao za mapato na ushuru (E1) za karibuni zaidi.
  • Bili ya stima, maji, au simu, au nakala ya mkataba wa kupangisha nyumba uliokwisha kutumwa kwa Huduma husika za Fedha za Umma (kuthibitisha unakoishi).
  • Stakabadhi rasmi inayoonyesha nambari yako ya bima ya kijamii (AMKA) k.m inayotolewa katika ofisi za KEP ama AMKA.
- Tahadhari kwa wataalam wa kujitegemea: Iwapo ulikuwa umejiajiri, utahitaji kutuma nakala za uamuzi wa kufunga biashara na Huduma ya Fedha za Umma na OAEE.

Shirika la PES lina haki ya kuitisha stakabadhi zozote linazodhania kuwa muhimu katika kufanya uamuzi wa ukosefu wa ajira.

Nitafanyaje upya kadi yangu ya OAED?

Kadi ya kutokuwa na ajira lazima ifanywe upya kila miezi mitatu. Unaweza kufanya hivyo katika tawi lolote la OAED kwa kuwasilisha pasi yako ya usafiri au kibali cha makazi au cha kazi. Kwa urahisi wako na kuepuka foleni ndefu katika ofisi za shirika, inapendekezwa utumie huduma za mtandao za kufanya upya kadi ya kutokuwa na ajira.

Ili kutumia huduma za mtandao za OAED kwa mara ya kwanza, unahitaji kuwa umejisajilisha awali katika mfumo huo. Unaweza kupata habari zote muhimu kutoka tawi moja mashinani na ufuate maagizo katika tovuti http://eservices.oaed.gr:7777/pls/apex/f?p=110

Mimi sina kazi ya imara kwa kuwa mimi ni mfanyakazai wa misimu. Je, ninahitimu kupata manufaa?

Ndio,ikiwa una bima na IKA na kufanya mojawapo ya taaluma zifuatazo.
Wanaofaidika wa manufaa ya msimu wa pekee ni wale wanaofanya kazi Ugiriki, wana bima na IKA – ETAM na hufanya mojawapo wa taaluma hizi:

  • mjengo,
  • kuchonga mawe,
  • Mtengeneza matofali,
  • kuchoma mawe,
  • potter,
  • mfinyanzi,
  • mkusanya gundi,
  • mfanyakazi wa tumbaku,
  • mwimbaji, mwanachama wa muungano wa kitaaluma,
  • fundi wa viatu,
  • mfanyikazi wa mwezi katika maeneo ya meli,
  • mchimbaji, muinuaji, ujenzi barabarani, na mwendesha mashine ya kuchimba
  • msanii,
  • fundi wa sinema au runinga,
  • fundi wa projekta au mdogo wake
  • mwekahazina katika sinema au ukumbi wa michezo,
  • mfanyikazi wa mwezi katika sekta ya utalii na upishi
  • Wafanyakazi wa Nasosi.

Masharti ya kupata manufaa ya muda

Ι wafanyikazi wa mjengo

  1. wawe wamemaliza kikamilifu siku 95 hadi 210 katika sekta ya ujenzi mwaka uliotangulia.
  2. Siku hizi, 20% inaongezwa pamoja na siku za mapumziko. Kimsingi, mwenye bima akimaliza kati ya siku 73 na 163 za kazi halisi anatosha kupewa marupurupu.
  3. Lazima wasiwe wanakandarasi, na wasiwe wameajiri zaidi ya watu watatu wa mshahara wa mwezi
  4. Kwa vyovyote vile lazima wafanye kazi katika taaluma yao.
  5. Wanaoshiriki katika mipangilio ya OAED na kupata faida ya elimu hawawezi kupata hii marupurupu. 13

13:aya.5a ibara ya 37 L.1836/89

ΙΙ Makundi mengine (kando na wafanyikazi wa mjengo)

  1. Kumaliza siku 50 hadi 210 za bima katika kalenda ya mwaka uliopita kunahitajika kabla ya malipo.
  2. Kwa wafanyakazi wa msituni – wakusanyaji gundi na wafanya kazi wa Nasosi, siku 50 hadi 240 za bima zinahitajika.
  3. Kwa wafanyakazi wa mshahara katika idara ya Utalii na Upishi, lazima wamalize walau siku 75 na sio zaidi ya siku 50 za kazi kati ya Oktoba 1 na Disemba 31 ya mwaka uliopita.
  4. kwa wachimbaji, wainuaji, watengenezaji barabara na opareta wa mashine nyinginezo, siku 70 hadi 210 za bima zinahitajika.
  5. Siku ambazo zilitumika katika taaluma za sekta nyingine katika mwaka uliotangulia malipo hazipaswi kuwa zaidi ya zile zimekamilishwa katika taaluma yako.
  6. Jumla ya siku za kazi katika mwaka uliotangulia malipo zisizidi siku 240.
  7. Iwapo kipindi cha malipo ya manufaa ya pekee ya msimu kitalingana na ile cha malipo ya faida za wasokuwa na ajira (OAED), basi manufaa ya kimsimu yanaondolewa na kiwango kutoka kwa wasokuwa na ajira.
  8. Wanaonufaika kutokana na programu za mafunzo za OAED hawawezi tena kufaidika na hii marupurupu. (aya 5a, ibara ya 37 L. 1836/89)

Kiwango cha marupurupu ya msimu maalum

  1. Kiwango cha marupurupu maalum kwa wafanyikazi wa mjengo huwa ni 70% ya mara 35 ya mshahara wa sasa wa mfanyikazi asiye na maarifa.
  2. Kiwango cha marupurupu maalum kwa wafanyakazi wa Nasosi huwa ni 70% ya mara 50 ya mshahara wa sasa wa mfanyikazi asiye na maarifa.
  3. Kiwango cha marupurupu maalum ya wafanyakazi wa msituni – wakusanyaji gundi, wafanyikazi wa tumbaku, wafinyanzi, wachonga mawe, na wafanyakazi wa maeneo ya meli wa mshahara wa mwezi hupata 70% ya mara 35 ya mshahara wa sasa wa mfanyikazi asiye na maarifa.
  4. kiwango wanachopata wanamuziki, waimbaji, waigizaji, opareta wa projekta za filamu, waweka hazina za sinema na filamu, mafundi wa sinema na runinga, wachimbaji, wapakuaji, opareta wa mashine za ujenzi wa barabara, wafanyikazi wa kulipwa katika sekta za utalii na upishi, hupata 70% ya mara 25 ya mshahara wa sasa wa mfanyikazi asiye na maarifa.

Stakabadhi ambatani

  1. Kutuma maombi kielektroniki – Tamko la dhati ambapo makundi husika hukiri mmoja baada ya mwingine kwamba:
      a) hushiriki kazi katika taaluma zao tu,
      b) hawashiriki mipangilio mingine ya mafunzo ya OAED, na ambayo sehemu yake kubwa hujumuishwa katika mwaka wa malipo,
      c) Kwamba wao si wanakandarasi kwa vyovyote, na kwamba hawajaajiri wa mishahara wapitao watatu (kwa wafanyikazi wa mjengo),
      d) Hawapokei pensheni kwa vyovyote, iliyo sawa au inayozidi kiwango cha chini cha pensheni ya uzeeni ya IKA-ETAM.
  2. Wanamuziki wanahitaji kupata vyeti kutoka kwa muungano wao wa wataalamu.
  3. Maopareta wa mashine mbalimbali (kama za kuinua) wanahitaji kuwa na leseni hitajika za kuendeshea mashine hizo.
  4. Unahitaji kuwa na akaunti ya benki katika Benki ya Kitaifa ya Ugiriki na kutuma nakala ya kitabu chako cha benki ambapo umeandikwa kuwa mfaidika wa kwanza. Malipo ya marupurupu kwa wanaonufaika hufanywa kwa akaunti za benki walizoandika katika fomu ya maombi ya kielektronikia – Tamko la dhati. Kwa sababu hii, ni muhimu kuwa makini na kutoa habari sahihi (IBAN, TRN, Nambari ya bima ya kijamii (AMKA), n.k.)

Kwa malipo ya marupuru haya, stakabadhi zifuatazo hutafutwa na idara ulikotuma maombi yako:

  • Kwa raia wa mataifa ya tatu, habari za kibali cha makazi huchukuliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani.
  • Ilani ya tathmini ya mapato na ushuru huchukuliwa na Katibu Mkuu wa Mifumo ya Habari (G.S.I.S).
  • Habari za bima hukaguliwa katika mfumo elektroniki wa IKA-ETAM.

Kipindi cha malipo ya marupurupu ya kimsimu

Marupurupu haya hulipwa kila mwaka kuanzia 10/9 -30/11.

Ninatafuta kazi kulinganaa na mahitaji, lakini pia kwa kuzingatia ujuzi wangu wa mambo yanayonivutia. Je, kuna njia maalum ya kutafuta kazi?

Ndio!
Mipangilio ya ushauri wa ajira ilianzia Ugiriki katika miaka ya karibuni, na husaidia watu wanaotafuta kazi kufikia matakwa ya soko la kazi. Wao hutoa usaidizi wa kibinafsi na habari kuhusu mbinu mwafaka zaidi za kupata kazi, na kusaidia katika uandika wa tawasifu na barua ambatani, usaidizi wa kitaaluma katika kutafuta kazi, na maandalizi ya mahojiano.

Huduma za ushauri wa ajira hutolewa na OAED (tazama hapo juu), Shirikisho la Taasisi za Wafanyikazi wa Ugiriki (INE GSEE) 14, IEK, KEK na KEE (tazama sura juu ya Elimu) na baadhi ya Mashirika yasiyo ya serikali.

    ➢ Ushauri! Daima kuwa mwangalifu na:
    • Matangazo ya kibiashara yanayoulizia wafanyikazi kwa misingi ya jinsia, rangi, umri, deni, uwezo wa kimwili, mielekeo ya kimapenzi au mitazamo ya maumbile, kwa sababu huo ni ubaguzi.
    • Matangazo ya kibiashara yasiyoelezea kinagaubaga wanachotaka na habari za mwajiri.

14:Kwa vijana (kuanzia miaka 16-30) wanaotafuta kazi, vituo vya kukuza ajira maalum (EKPA) vya INE GSEE huendeshwa katika miji mitatu mikubwa zaidi ya Ugiriki (Atheni, Thessaloniki, Patrasi) na hutoa huduma kwa njia ya mtandao, kupitia tovuti: www.ekpaine.gr

anwani muhimu

Unaweza kupata anwani muhimu na nambari za mawasiliano za mashirika mengine kando na OAED yanayotoa huduma za ushauri katika orodha ifuatayo:

ATHENI

EKIPA YA ATHENI
    Anwani: 71Α Em. Mt. Benaki., P.C. 10681, Atheni
    Tel.: 210 3327768
    Barua pepe: athina@ekpaine.gr
Muundo wa Usawa wa Kijinsia (INE GSEE)
    Anwani: 87-89 Mt. Solonos., Atheni
    Tel.: 2103637756 - 2103637767
    Barua pepe: isotita@poeeyte.gr
    (kwa wanawake wanaofanya kazi na waliopoteza kazi)
Kituo cha kuajirika cha PRAKSIS
    Anwani: Kituo cha Mshikamano cha Atheni (Jumba la zamani la Frourachio), 2 Mt. Domokou. & Mt. Filadelifeia, orofa ya pili, mkabala na kituo cha Larissa
    Tel.: 2108210551
    employability@praksis.gr
-PRAKSIS – Kituo cha Kutwa cha Chokoraa
    Anwani: 26-28 Mt. Deligiorgi, Metasourigio, Atheni
    Tel.: 2105244574, 2105244576, 2105244578
Shirika lisilo la Serikali la Ε.Κ.Pο.S.P.Ο NOSTOSI, dhidi ya ubaguzi wa kijamii na ukosefu wa ajira
    Anwani: Metsovou & Mt. Notara, Esachia
    Tel:2108815310, 2105225486 / Fax: 210 5221950
    Barua pepe: nostos@ath.forthnet.gr
    Saa za kazi: 09:00-17:00
- PEPSAEE – Kituo cha usaidizi wa kiakili na kijamii na ukosefu wa ajira kwa muda mrefu
    Anwani: 22 Mt. Papanastasiou., Egaleo (karibu na kituo cha “Egaleo”)
    Tel:2108224674 - 2105989340
    Barua pepe: menoenergos@pepsaee.gr
- Kituo Maalum cha Kutwa ‘Kituo cha mazungumzo ya kijamii”
    41 Mt. Epirou., Atheni, P.C. 104 39
    Τ. 210 8818946
    F. 210 5245302
    Barua pepe. ekhkkd@pepsaee.gr

THESALONIKI

- EKIPA YA THESALONIKI
    Anwani: 24 Esopou & Mt. Promitheos., orofa ya 3, P.C. 54627, Thesaloniki
    Tel.: 2310 545113
    Barua pepe: thess@ekpaine.gr
OFISI YA AJIRA YA THESALONIKI
    Anwani: Α1 Mt. Vasileos Georgiou, P.C. 54640, THESALONIKI
    Tel.: 2313317583, 2313317548-50
    Barua pepe: grafeioergasias@thessaloniki.gr

PATRASI

EKIPA YA PATRASI
    Anwani: 20 Mt. Kolokotroni. (orofa ya 6), P.C. 262 21, Patrasi
    Tel.: 2610 624755
    Barua pepe: patra@ekpaine.gr

Rudi
Mradi wa 1.4.b/13 ‘Matangazo ya Redio ya masuala kuhusiana na wahamiaji, uzazi, na usambazaji mpana wa vifaa vilivyochapishwa, vya sauti na vielelezo’ ulifadhiliwa 95% na Hazina ya Jumuiya na 5% na Rasilimali za Kitaifa