Kutokana na upekee wa upeo wa ardhi ya Ugiriki na visiwa vyake vingi, malengo yameeelekezwa sio tu kwa uchukuzi wa barabarani, bali pia kwa usafiri wa majini.
Usafiri wa masafa marefu nchini Ugiriki hutolewa na: Treniusafiri:
Nchini Ugiriki kuna usafiri wa majini unaounganisha bandari kubwa za bara na visiwa, ukiwahudumia maelfu ya wenyeji na watalii, hususan wakati wa majira ya joto.
oKuondoka/kuwasili kwa mashua | Tel. 14944 |
Bandari ya Piraeusi | Tel. 2104226000, (www.olp.gr) |
Bandari ya Rafina | Tel. 2294022300, 2294022481 |
Bandari ya Lavurio | Tel. 2292025249 |
Bandari ya Agiosi Konstantinosi | Tel. 2235031759 |
Mfumo wa uchukuzi wa umma wa Atheni hujumuisha mfumo wa chini ya ardhiwa reli (Metro), tramu, mabasi na troli, huku sehemu ya huduma za usafiri zikishughulikiwa na Reli ya Vitongoji vya Jiji. Katika sehemu zingine za Atika, huduma nyingi zaidi za uchukuzi hutolewa na kampuni ya KTEL iunganishayo miji, na sehemu ilosalia ikisimamiwa na reli ya vitongoji na mabasi ya mjini.
Shirika la Uchukuzi wa Mjini la Atheni (OASA) husimamia sehemu kubwa ya wilaya, huku matawi yake, Uchukuzi wa Barabarani SA (OSY) na Uchukuzi wa Reli Mjini SA (STASY) husimamia utekelezaji wa usafiri, na kuna ushirikiano na TRAINOSE SA, kutokana na kuwepo kwa sehemu ya tovuti wake (Reli ya Vitongoji) ndani ya mfumo wa miji ya Atheni. Kwa wilaya nyinginezo, usimamizi wa usafiri umekabidhiwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafri wa Abiria, na utekelezaji wake hufanywa na KTEL Atika SA.
Kwa habari zaidi zinazohusiana na ratiba za uchukuzi wa umma, angalia vituo maalum vya simu na tovuti zao:
Katika Patra, usafiri wa mjini husimamiwa na KTEL. Vitongoji vya Patra hutumia treni za miji (Proastiakos), ambazo ziko chini ya usimamizi wa TRAINOSE, zikiunganisha Patra na Rio pamoja na vitongoji vinginevyo vya jiji.