Baraza la Mawaziri, ambalo lina wajumbe wa Serikali hujumuisha Waziri Mkuu na Mawaziri wote walioteuliwa na Rais wa Jamhuri, na kupendekezwa na Waziri Mkuu.
Kwa kawaida, Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa chama kinachodhibiti wingi mkubwa wa Wabunge. Iwapo hakuna chama chenye wingi mkubwa wa Wabunge, Rais humpa kiongozi wa chama chenye wingi kidogo wa Wabunge mamlaka ya kutathimini, k.m. anampa idhini ya kutathmini uwezekano wa kuunda serikali kupitia muungano wa vyama vingine ambavyo vinaweza kupata kura ya imani bungeni. Chini ya Katiba, Waziri Mkuu atakuwa mlinzi wa umoja wa serikali, na kwa hivyo kuelekeza shughuli zake. Waziri Mkuu basi atakuwa mtu mwenye mamlaka zaidi katika mfumo wa siasa za Ugiriki, na atapendekeza uteuzi au kuachishwa kazi kwa Mawaziri na Manaibu wao kwa Rais wa Jamhuri.
Demokrasia ya Bunge la Kigiriki imekita msingi katika kanuni ya imani iliyotangazwa na Bunge kwa Serikali. Kwa hivyo Rais lazima ateue Waziri Mkuu ambaye atapoke kura ya imani ya Wabunge (kura 151). Serikali inaweza kwa wakati wowote kuomba kura ya imani kutoka Bunge. Kwa upande wake, baadhi ya Wabunge wanaweza kuomba ‘kura ya kushutumiwa’. Taratibu hizi mbili huwa ni nadra kutokea.