Ugiriki ina visiwa takribani 2,500. Kati ya visiwa hivi, ni 165 ambavyo watu wanaishi:
Visiwa vingi vinapatikana Eejeni, na vimegawanyika katika sehemu saba (kutoka kaskazini hadi kusini):
- Visiwa vya kaskazini mashariki mwa Eejeni: Agiosi, Efustratiosi, Thasosi Ikaria, Lesibosi, Limnosi, Oinousesi, Samosi, Samothuresi, Chiosi, Pusara
- Siporadesi: Alonisosi, Skiathosi, Sikopelos, Skairosi
- Yuboea
- Visiwa vya Saronika: Ajistiri, Eejina, Methana, Porosi, Salamina, Sipetisesi, Haidura
- Saikiladesi: Safu ya visiwa 56, hususan Amorigosi, Anafi, Andurosi, Antiparosi, Delosi, Iosi, Tizia (Kea), Kimolosi, Kithinosi, Milosi, Mikonosi, Nakusosi, Parosi, Santorini, Serifosi, Sikinosi, Sifunosi, Sirosi, Tinosi, Folegandurosi, na zile saikaledi ndogo zinazojumuisha
• Donousa, Irakileia, Koufonisia, na Sikoinousa.
- Dodekanesi: Asitipalaia, Kalimunosi, Karipathosu, Kasosu, Kasutelorizo, Kosu, Leipusoi, Lerosi, Nisirosi, Patimosi, Rodesi, Simi, Tilosi, Chalaki
- Krete
Bahari ya Loniani huwa na safu moja tu ya visiwa:
Visiwa vya Loniani: Zante, Ithaki, Korfu, Kefalonia, Lefukada, Pasoi na Kithira, ambavyo vinapatikana mkabala na Peloponesi, ndivyo vikubwa zaidi kati ya visiwa vya Loniani, na huunda Epitanesi. Visiwa vingine vy Loniani ni pamoja na: Antipakisoi, Antikithira, Ereikousa, Kalamosi, Kasitosi, Mathiraki, Meganisi, Othonoi, Sikoripiosi, Sitirofadesi.
Visiwa ambavyo si sehemu ya safu yoyote ya visiwa, lakini vyenye fahari ya uzuri wa asili, ni pamoja na visiwa vya Gavudosi (Kusini mwa Krete), Elafonisosi (katika Ghuba ya Lakoniki), na Trizonia (katika Ghuba ya Korintho).
Baadhi ya ustaarabu kongwe zaidi za Ulaya zimeendelezwa katika visiwa vya Ugiriki (Sikiladiki, Minoiki, nk.). Visiwa hivi vina maeneo ya kipekee ya akiolojia, na urithi wa mila haiba za utamaduni maridhawa wa kudumu.