Ugiriki, ambayo kirasmi ni Jamhuri ya Heleniki, ni taifa lililo Kusini mashariki mwa Ulaya, katika upembe wa kusini wa Peninsula ya Balkani, ya Mashariki mwa Mediterenia. Katika orodha ya nchi za dunia kulingana na ukubwa wa maeneo yake, Ugiriki inaorodheshwa ya 97 kati ya mataifa 249. Jiji kuu la Ugiriki, na ambalo ni mji mkubwa zaidi nchini, ni Atheni. Miji mingine mikubwa ni Wathesaloniki, Patra, na Heraklioni.
Ugiriki ina historia ndefu na nzuri, wakati ilikuwa na ushawishi mkubwa wa kiutamaduni katika mabara matatu – Ulaya, Afrika, na Asia. Na kama kiini cha ustaarabu, Ugiriki imeathiri na ingali inaathiri sehemu kubwa ya historian a maendeleo ya sasa. Ugiriki ya kale ndiyo kitovu cha demokrasia na falsafa, historia, dawa, Michezo ya Olimpiki, uigizaji, tanzia na vichekesho (futuhi).
Ugiriki ilijishindia uhuru mwaka wa 1830. Imekuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya (zamani ikiwa Jumuiya za Ulaya) tangu mwaka 1981, Yurozoni tangu mwaka 2001, na Mkataba wa Ushirika wa Mataifa ya Kaskazini mwa Atlantiki (NATO) tangu mwaka 1952. Aidha, ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa (1945).
Ugiriki ina eneo bara kubwa, sehemu ya chini ya kusini mwa Balkani, inayounganisha iliyokuwa Peloponisi na shingo la Korintho. Tangu wakati wa ujenzi wa Mfereji wa Korintho, Peloponisi imekuwa kisiwa.
Mipaka ya nchi ya taifa la Ugiriki ni Albania upande wa kaskazini magharibi, Bulgaria, na iliyokuwa jamhuri ya Yugosilavia ya Masedonia kwa upande wa kaskazini, na Uturuki upande wa kaskazini mashariki. Pia imezungukwa na Bahari ya Aajeni upande wa mashariki, na Bahari ya Libya upande wa kusini. Taifa la Ugiriki linashikilia nafasi ya 11 katika orodha ya nchi zenye kanda ndefu za pwani, ikiwa na ukanda wa kilomita 13, 676, pamoja na viswa takribani 2,500. Kati ya visiwa hivi, ni 165 ambavyo watu wanaishi.
Nyanda kubwa zaidi ni zile za Larisa katika Thesali na Jayanisa katikati mwa Masedonia.
Kijiografia, Ugiriki imegawanya katika mikoa 9, ambayo imegawanywa katika wilaya 51. Mikoa Hizi ni :